WAPENZI NA MASHABIKI WA MBEYA CITY FC WAVUNJA VIOO YA MAGARI YA TIMU YA TANZANIA PRISONS NA KUMUUMIZA MCHEZAJI MMOJA.










Matokeo ya wanafunzi wa sekondari yataanza kupangwa kwa kutumia COURSE WORK zao!


Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalalusesa ameliambia gazeti la Habari Leo kuwa Serikali itabadili mfumo wa upangaji alama za ufaulu wa mitihani ya Sekondari ili kazi anazofanya mwanafunzi shuleni, zitumike katika kumpatia alama ya ufaulu katika mtihani wa mwisho, mfumo unaolandana na ule unaotumika katika Vyuo Vikuu.
Tayari Serikali imetuma dokezo, ambalo lipo katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa wadau wa elimu ili kupata maoni
yao kabla ya kuanzisha mfumo huo. Dodoso hilo limeeleza kuwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi zitachangia asilimia hamsini na mtihani wa mwisho utachangia asilimia hamsini pia.
Mathalani, kwa mtihani wenye alama za jumla ya 100, mwanafunzi akipata alama 50 kupitia kazi za shule, atatakiwa kutafuta alama 50 katika mtihani wa mwisho.
Kwa kutumia mfumo huu, mwanafunzi atakuwa anakwenda kufanya mtihani akiwa tayari anajua alama za mchango wa kazi shuleni (continuous assessment) na kuwa na hakika ya anachotakiwa kukipata wakati anakwenda kufanya katika mtihani:
“Hatutaki kuona mwanafunzi hanufaiki na kile alichokivuna akiwa shule. Mfano mfumo wa sasa mwanafunzi aliyepata alama F ni aliyepata alama kati ya 0-34.
“Hata hivyo, kumekuwa na mitizamo, maoni na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi. Mfumo huu hata hivyo hautumiki kwa wanafunzi wa kujitegemea,” lilieleza dokezo hilo.

RAY C WAZICHAPA NA NORA STUDIO..KISA NORA KUVAMIA GEMU YA MUZIKI


KATIKA hali ya kushangaza, siku chache baada ya kuripotiwa kupona na kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ anadaiwa kugeuka mwanamasumbwi na kumpa kipigo mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.
Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wiki iliyopita ndani ya studio moja ya kurekodia muziki iliyopo Kinondoni, Dar ambapo wawili hao walikutana walipokwenda kurekodi ngoma zao.
Ilidaiwa kuwa akiwa studio hapo, Nora alikutana na Ray C ambaye pia alizama mahali hapo bila mawasiliano na prodyuza anayemtengenezea ngoma mpya.

Chanzo hicho kilipasha kuwa baada ya Ray C kuingia studio hapo alimkuta prodyuza huyo akiandaa ngoma ya Nora ambapo alihoji kilichompeleka mwigizaji huyo mahali hapo.
Ilidaiwa kuwa prodyuza huyo ambaye jina halikupatikana alimwambia Ray C kuwa Nora alifika kurekodi wimbo wake.

Ilisemekana kuwa Ray C hakuridhishwa na majibu hayo, akaomba asikilizishwe ngoma hiyo ya Nora lakini baada ya kusikiliza ilidaiwa kwamba Ray C aliiponda mbele ya Nora, jambo ambalo mwigizaji huyo hakufurahishwa nalo.
Ilidaiwa kuwa Nora alipandwa hasira na kujikuta akimjibu mbovu Ray C.

Habari ziliendelea kutiririka kuwa siku hiyo walimalizana kwa kusonyana na siku iliyofuta walikutana tena studio hapo ambapo Ray C alidaiwa kutinga akiwa ‘masanga’.
Ilisemekana kuwa alipomuona Nora alianza kumpa vijembe, jambo lililosababisha Nora kushikwa hasira ndipo wakavaana na kuzichapa.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Ray C ndiye aliyeibuka bingwa wa ndondi hizo kwa kumtwanga Nora hadi kumvimbisha jicho kabla ya maprodyuza na watu wengine kufanya kazi ya ziada kuwaamulia.
Ilisemekana kuwa baadaye Ray C alitolewa nje ndipo akahamishia hasira kwenye gari la Nora aina ya Toyota Vitz kisha akalivunja kioo na kutambaa zake.

Baada ya kupenyezewa ‘niuz’ hizo gazeti hili lilimtafuta Nora ambaye alikiri kutokea kwa sekeseke hilo huku akibainisha namna alivyoumizwa jicho lake na kuvunjiwa kioo cha pembeni cha gari lake.
Aliongeza kuwa siku hiyo alipoteza pochi wakati wa ugovi huo.

“Ray C alinikuta studio nikifanya wimbo, kilichonishangaza baada ya kuniona tu alibadilika ghafla.
“Nilijua angenishauri kwa kuwa ndiyo ninaanza gemu kumbe mwenzangu alifikiria vingine,” alisema Nora na kuongeza:
“Mbali na kuniumiza jicho lakini alinifanyia mambo ya ajabu sana, kama kusingekuwa na watu wa kutuamulia basi chochote kingetokea.

“Sikwenda kuripoti polisi. Niliamua kusamehe kwa sababu kuna watu walinisihi niachane naye kwa sababu bado kuna mambo yanamwendesha.
Kwa upande wake Ray C alitafutwa kwa kila njia kupitia simu ya mkononi na kumvizia studio lakini hakupatikana hivyo juhudi za kumpata zinaendelea

HUU NDO UTAJIRI WA WEMA SEPETU.



Well, well, well! Hiki ni kitu ambacho kila mmoja anapenda kukifahamu. Wema Sepetu ni tajiri kiasi gani? Ni ngumu kusema exactly mrembo huyu ana shilingi ngapi benki, lakini mambo anayofanya yanatupa jibu la wazi kuwa, Wema ana mkwanja mrefu. So hebu tuangalie mangapi makubwa yaliyohusisha fedha nyingi aliyoyafanya kuanzia mwezi June, 2012.
IMG_4951
1. Thamani ya nyumba yake

Wema Sepetu aliwaacha hoi watu wengi baada ya kuonesha nyumba yake mpya exclusively kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV. Alisema thamani ya nyumba yake hiyo ilifikia shilingi milioni 400 na hiyo ni tofauti na karibu shilingi milioni 30 za kuipamba ndani. Hiyo ilikuwa ni tarahe za mwanzo za mwezi June, 2012.
Sebule
Sebule
Wema Sepetu akielezea jambo
Wema Sepetu akielezea jambo
Wema na Zamaradi Mketema wa Clouds TV
Wema na Zamaradi Mketema wa Clouds TV
912
Sehemu ya nje ya nyumba
Sehemu ya nje ya nyumba
616
Dj Choka alikuwa miongoni mwa watu waliotembelea nyumba hiyo
Dj Choka alikuwa miongoni mwa watu waliotembelea nyumba hiyo
2. Uzinduzi wa filamu yake Superstar

Katika historia ya Bongo Movies, hakuna filamu iliyowahi kuwa na uzinduzi wa nguvu kama wa filamu ya Wema ambayo hata hivyo haijawahi kutoka, Supastar. Katika uzinduzi huyo, Wema alimdondosha muigizaji namba moja wa kike nchini Nigeria, Omotola Jalade ambaye alimpeleka kwenye event iliyofanyika Giraffe Hotel Ocean View ambako watu mbalimbali walikutana kubadilishana mawazo na Omotola. Hiyo ilikuwa ni baada ya kushindwa kufika kwa wakati.
IMG_6117
Awali ulifanyika uzinduzi wa filamu hiyo yenye mastaa kibao akiwemo yeye mwenyewe, TID, Shetta, Mwinyi Machozi, Chaz Baba, Barnaba na wengine kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro ambako mastaa wote wa orodha A nchini walihudhuria huku Shaa na Shilole wakiwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza.
DSC_0075
Ben Kinyaiya na Irene Uwoya
Ben Kinyaiya na Irene Uwoya
Ray, Dr Cheni, Steve Nyerere nao walihudhuria
Ray, Dr Cheni, Steve Nyerere nao walihudhuria
DSC_0172
Shughuli nzima hiyo iliyofanyika mwishoni mwa mwezi June mwaka jana, ilitumia takriban shilingi milioni 40 zikiwemo gharama za kumlipa Omotola.

3. Gari anayomiliki
Kwa sasa Wema anamiliki gari aina ya AUDI Q7 ambayo thamani yake inafikia shilingi milioni 80. Awali ya hapo alikuwa na Toyota Mark X ambayo thamani yake ni takriban shilingi milioni 60.
Wema akiwa na mkoko wake
Wema akiwa na mkoko wake
4. Thamani ya ofisi na kampuni yake, Endless Fame Films
February 21, Wema alifanya uzinduzi maalum wa ofisi za kampuni yake ya Endless Fame Films zilizopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambazo thamani yake ni takriban shilingi milioni 70.
DSC_1824
off12-600x600

5. Gharama anayotumia kuwatunza mbwa wake, Vanny na Gucci

Mtandao wa Global Publisher jana uliandika, “KWA wale wenye hali ngumu kimaisha wataishia kusema; ni kufuru iliyoje kwani staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu hivi karibuni amewafanyia mbwa wake wawili ‘shopping’ iliyogharimu dola 4,000 za Kimarekani (zaidi ya Sh. milioni 6.5 za madafu).

Wema aliteketeza kiasi hicho cha fedha kwa kuwanunulia mbwa hao pafyumu, viatu na nguo, alivyoagiza kutoka nchini China, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaishi katika mazingira mazuri.

Akizungumzia ‘shopping’ hiyo nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar, Wema alisema: “Kiukweli nawapenda sana hawa mbwa, ukinipasua roho yangu utawakuta ndiyo maana nataka wavae na kunukia vizuri, kinyume chake siwezi kuwa na amani.
0caeb4ac921811e28e6622000a9f0a1a_7
Vanny na Gucci wakicheza
Vanny na Gucci wakicheza
83b019e2914b11e28e0922000a9f1335_7
818e18e0921c11e2af9022000a1f9a23_7
90197700921811e2996f22000a1fbc6f_7
Vanny
Vanny
Vanny
Vanny
Gucci akiwa amelala
Gucci akiwa amelala

“Najua watu wanaweza kushangazwa na kitendo cha mimi kutumia kiasi hicho cha fedha lakini sioni kama ni tatizo kwani ni kitu ambacho kinanipa furaha katika maisha yangu.”

Leo kupitia Instagram, Wema ameandika, “Vanny ake heading to da hospital…. my poor baby is sick…. nat happy at all, hope u get better soon.”

6. Shilingi milioni 13 alizomtolea Kajala baada ya kusomwa hukumu yake

Jana Wema Sepetu alimake headline baada ya kutoa mfukoni mwake shilingi milioni 13 kulipa faini aliyopigwa muigizaji mwenzie Kajala Masanja aliyehukumiwa jana kwenda jela miaka mitano ama kulipa kiasi hicho cha fedha.

Akizungumza exclusively na Bongo5, Wema amesema hakufikiria mara mbili kutoa kiasi hicho cha fedha.
“Kusema kweli wanasemaga kwamba kutoa ni moyo so naamini what I did is best, nimetoa kwasababu I had to do it and sikuthink twice kuhusu kufanya hivyo,” amesema Wema.


“Nimefanya kama namsaidia rafiki yangu kama namsaidia ndugu yangu na sidhani kama ingekuwa ni kitu kizuri kumuona mwenzako anaingia kwenye dhahama, kwenye tabu, kwenye mateso na wakati nina uwezo wa kumsaidia kwahiyo I just did what I had to do.”
7. Jinsi anavyomwaga hela kwenye sherehe mbalimbali

Katika katika sherehe za 8020 Fashion’s Woman Celebration zilizofanyika kwenye siku ya wanawake duniani, Wema aliuteka ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kumwaga mihela kwa mwimbaji maarufu wa Taarabu nchini, Khadija Omar Kopa. Wema alimwaga mkwanja huo kumpongeza Khadija kwa kukonga moyo wake.

Hayo ni machache tu tunayofahamu na kwa hesabu hizo bila shaka utakubaliana nasi kuwa Wema Sepetu ana mkwanja mrefu!!!

DIAMOND BHANA NOOMA SAAAAANA ! ONA ILIVYOKUA FIESTA JANA!

HALI ILIVYO KATIKA MSIBANI KWA BABA YAKE WEMA MAREHEMU BALOZI ISAAC SEPETU


Mama mzazi wa Wema akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe mzee Sepetu.
 
Kajala Masanja (kushoto), Wema Sepetu (katikati) na Zamaradi Mketema (kulia) wakiwa katika hali ya majonzi nyumbani kwao Wema Sepetu, Sinza - Mori jijini Dar.

Kajala Masanja (kushoto) na Wema Sepetu (katikati) wakiangua vilio. Kulia Zamaradi akijaribu kumtuliza Wema.
Ndugu wa karibu wa marehemu akiwa na simanzi nzito.
STAA wa sinema za Kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Isaac Sepetu, bado yuko kwenye wakati mgumu baada ya jana asubuhi kupatwa na msiba mkubwa wa kuondokewa na baba yake mzazi Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki asubuhi ya leo.
Kwa sasa kuna watu wengi wamefika kumjulia hali maeneo ya Sinza, Mori jijini Dar, rafiki yake wa karibu Kajala Masanja na Zamaradi Mketema wapo bega kwa bega kuwa naye karibu na vilio vimetawala kila kona ya familia ya marehemu Balozi Sepetu.

Bado haijafahamika mazishi yanafanyika lini maana wanasubuliwa watoto wa Marehemu Tunnu Sepetu na Sunna Sepetu ambao wanaishi nchini Marekani, lakini kuna tetesi kuwa huenda mazishi hayo yakafanyika siku ya Ijumaa.
Mama mzazi wa Wema bado yuko kwenye hali ya huzuni baada ya kufiwa na mume wake ambaye amedumu nae kwa miaka mingi kabla ya kupatwa na mauti asubuhi ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar. Mpaka mauti yanamfika, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na kiharusi.

NOMA SANA MCHUMBA WA MTU ANASWA LIVE AKIJIUZA...AZIMIA NA KUTOKWA MAPOVU BAADA YA KUNASWA KWA "KIMBOKA "


Mchumba huyo wa mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Diva alitoa kali ya mwaka baada ya kuzimia ghafla huku akitokwa na mapovu kinywani baada ya kunaswa na OFM akijiuza.
Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita maeneo ya Kimboka, Buguruni, Dar ambapo msichana huyo pamoja na ‘madadapoa’ wenzake walikuwa wakifanya biashara hiyo haramu bila kificho.
Mara baada ya kuona wenzake wakiwa mikononi mwa nguvu za dola katika kamatakamata ya polisi, mrembo huyo ambaye baadaye alijitambulisha kama mchumba wa mtu, alianguka ghafla na kuzimia kiasi cha kuzua hofu miongoni mwa machangu wenzake walioangua kilio wakidhani mwenzao amekata ringi (kufa).
Baada ya muda msichana huyo alirejewa na fahamu akiwa mikononi mwa polisi na kuanza kuangua kilio akiomba asikamatwe kwa kuwa yeye ni mchumba wa mtu na atakuwa kwenye wakati mgumu kama mchumba’ke atajua anajiuza.

“Naomba msinikamate. Mimi ni mchumba wa mtu afande. Mtaniweka kwenye wakati mgumu kama akijua nilikuwa nikijiuza. Jamani nitamkosa mchumba wangu Luka,” alisema mrembo huyo huku akiomba maji ya kunywa.
Hata hivyo, kilio chake hakikuwazuia ‘OFM’ kufanya kazi yake ndani ya Kituo cha Polisi Buguruni, Dar  ambapo watuhumiwa hao wanasubiri kupandishwa kizimbani kwa ajili ya taratibu za kisheria