Chelsea boss to make stunning £50 million move for tricky superstar!

Wednesday, August 21, 2013 | comments


There has been some reports circulate which have claimed Chelsea boss Jose Mourinho will switch his attentions to Liverpool striker Luis Suarez if he fails to nail down top target Wayne Rooney.

The Uruguayan is a long-shot option but could yet move up the wish list.

Rooney came on for 28 minutes in United’s 4-1 demolition of Swansea and had a hand in two of the goals.

But he noticeably did NOT celebrate with his team-mates and is clearly desperate to get away. (Daily Mirror)

There has been some quality players linked with Chelsea and it will be interesting to see just who fans would like to see arrive?

Waingereza washambuliwa Zanzibar

Waingereza washambuliwa Zanzibar

 8 Agosti, 2013 - Saa 13:28 GMT
  • Google+
  • Chapisha
Ni mara ya kwanza kwa shambulizi kama hili kutokea Zanzibar
Polisi katika kisiwa cha Zanzibar wamesema wanawake wawili wa Uingereza wamerushiwa maji ya Acid katika nyuso zao baada ya kuvamiwa mwendo wa usiku.
Naibu kamishna wa polisi amesema kuwa wanaume wawili waliwatendea wanawake hao Katie Gee na Kirstie Trup, wote wenye umri wa miaka 18 kutoka London,kitendo hicho walipokuwa wakitembea katika barabara za mji wa kihistoria wa zanzibar.
Wanawake hao ni walimu wa kujitolea wakifanya kazi kisiwani humo
Amesema kuwa polisi tayari wameanzisha msako dhidi ya wanaume hao.
Katika taarifa yake shirika la usafiri la i-to-i nchini Uingereza lilisema kuwa wanawake hao wameondoka hospitalini.
Kwa upande wake wizara ya mambo ya ndani Uingereza ililezea wasiwasi kuhusu mashambulizi dhidi ya raia wake na kuwa tayari imetoa msaada kwao kupitia kwa ubalozi wake.
Wanawake hao, wanasemekana kufanyia kazi shirika moja la kujitolea na nia ya shambulizi hilo haijulikani.
Polisi wanasema kuwa wanawake hao wenye umri wa miaka 18 walikuwa wakitembea katika mji wa Mawe kisiwani Zanzibar ambao ni kivutio kikuu cha utalii kisiwani humo, wakati wanaume wawili waliokuwa wamepanda piki piki walipowamwagia Acid kwenye mikono , vifua na nyuso zao.
Wanawake hao walipelekwa kwa ndege hadi Dar es Salaam ambako walipokea matibabu . Afisa wa wizara ya afya amesema kuwa majeraha yao si ya kutishia maisha .
Polisi wa Zanzibar wamesema ni mara ya kwanza kwa raia wa kigeni kushambuliwa kwa namna hiyo na kwamba wanawasaka wahusika.
Zanzibar ni kisiwa kinachokaliwa na idadi kubwa ya waislam na shambulio hilo linakuja katika kipindi cha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan , wakati watu wakisherehekea sherehe za Eid

TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU HABARI ILIYOANDIKWA KATIKA GAZETI LA NIPASHE LA TAREHE 05 AGOSTI, 2013 INAYOSOMEKA “ELIMU: AIBU, AIBU”

TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU HABARI ILIYOANDIKWA KATIKA GAZETI LA NIPASHE LA TAREHE 05 AGOSTI, 2013 INAYOSOMEKA “ELIMU: AIBU, AIBU”

Katika gazeti la Nipashe la leo Jumatatu tarehe 5 Agosti, 2013 toleo Namba 057834 ukurasa wa mbele na wa nne kuna habari inayosomeka “Elimu: Aibu, aibu”. Katika habari hii mwandishi anaelezea kwamba kuna Madudu zaidi yamebainika katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, baada ya kuwapanga baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano kwenye shule ambazo hazina masomo ya michepuo yao.

Habari hiyo imenukuliwa kimakosa kutoka katika Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambapo imepotosha ukweli wa Taarifa husika. Usahihi wa Taarifa yenyewe ni kwamba wanafunzi waliobadilishiwa shule ni wale walioomba wenyewe kubadilishiwa michepuo (combination) na si kwamba walibadilishwa kutokana na kukosa michepuo waliyopangiwa awali katika shule hizo.

Aidha, wanafunzi wengine waliobadilishiwa shule ni wale waliopangwa mbali kutoka sehemu wanazoishi, walio wagonjwa wanaohitaji kuwa karibu na hospitali na walioomba kupangwa katika shule za kutwa kutokana na sababu za kiuchumi.

Wizara huwapanga wanafunzi wa Kidato cha tano kwa kufuata Taarifa zilizojazwa na wanafunzi wenyewe kwenye Selection Form (SEL Form) ambapo wanafunzi wanajaza machaguo yao kulingana na matarajio yao.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza matokeo ya kupangwa Kidato cha 5 wanafunzi waliohitimu kidato cha 4 mwaka 2012 tarehe 10 Julai, 2013. Baada ya tangazo hilo, Wizara ilipokea maombi ya wanafunzi wanaotaka kubadili shule au machaguo (combinations) walizopangwa kwa sababu mbalimbali. Wizara ilitafakari maombi hayo na kufanya mabadiliko ya shule/ machaguo.

Picha: Army Nando akiwa na mama yake mzazi LA, Califonia mara baada ya kutolewa katika mashindano hayo


Baada ya kutolewa katika mashindano ya BBA 2013,kwa kukiuka sheria za Biggie na kukutwa na kisu, mkasi pamoja na maneno ya vitisho dhidi ya mshiriki kutoka Ghana (Elikem), Army Nando ameshatua LA, Califonia, na kukutana na mama yake mzazi "Nancy Assenga" ambae pia ni meneja wake pamoja na mkurugenzi wa Swahili TV "Alex Kasuwi"


Nando akiwa na mama yake mzazi



kutoka kushoto ni Mayor wa LA, Deo Temba, Army Nando, Nancy Assenga (Mama mzazi na manager wake) pamoja na mkurugenzi mtendaji wa Swahili TV Bwana Alex Kassuwi