Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO''
ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la
kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia
yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au
kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka
comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.
![]() |
Msami na mkewe mpenzi Adela. |
"Posta mia hamsini, posta mia hamsini, usivue viatu viatu siti za kulala.. eeh chap chap ndege inaondoka hiyo hakuna kulemba".
Ni sehemu ya maneno ambayo inanijia akilini kumuona Joseph Nichodemus
Msami, akiwa kondakta. Sipati picha inakuwaje, lakini ndo hivyo KWA TAARIFA YAKO,
Kabla ya haujaanza kutamani kuwa kama yeye ni kwamba pamoja na hapo
alipo hivi sasa, Msami ameshafanya kazi ya ukondakta, kuvusha watu
kwenye madimbwi kipindi cha mvua maeneo ya sinza, kufundisha driving
school, na hata hivi karibuni akiwa BBC, kufanya kazi ya bodaboda.
Pamoja na changamoto ya maisha, Msami hajawahi kukata tamaa, anaeleza
jinsi maisha yalivyokuwa magumu wakati nikichat nae alipotinga katika
mojawapo ya ofisi za GK, za kaskazini, Arusha (nyingine ikiwa London, na
nyingine ikiwa Dar es Salaam)
Ebwana kuna siku mvua inanyesha halafu sasa mteja ni kibonge kuliko
mimi, na inabidi nimvushe kwenye dimbwi na hapo sina viatu vya kujiking
navyo, si unaijua Sinza ilivyo, full madimbwi kipindi hicho. Kulipa
inalipa, sema sasa cha moto utakiona. Anaeleza, Msami, hapa Napata
picha ni nafuu kiroba cha mchanga kuliko uzito mwingine wa walioshiba
vema.
Na siku moja kwenye basi kuna mzee mmoja alikuwa ndani, sasa mi
nakusanya nauli, anajifanya kuniongelesha kiingereza tu, ha, nilipoona
anazidi nami nikaamua kumpa kiigereza change, na nilipoona abiria
wengine wananisikiliza, nikapata maconfidence zaidi. Nilimpelekesha yule
mzee na kiingereza change cha certificate mpaka akasalimu amri.
Na siku nyingine pia kama kawaida kwenye ruti za daladala, kuna jamaa
akapanda alikuwa ni mwandishi wa habari, sasa kwa sababu nilishasoma
certificate tayari, na yule mtu namfahamu, aisee ikabidi niishushe kofia
chini taaaap, afu ndo nikamgongea nauli, ilikuwa noma sikutaka anione.
![]() |
Msami akiwa na field work Umaasaini, mkoani Manyara. |
KWA TAARIFA YAKO, wanafunzi walikuwa marafiki zangu, sikuwa na
ugomvi nao, hicho ni kitu muhimu, na kwa makondakta wengine, usione tabu
kufanya hiyo kazi il mradi unajua siku moja utakuja kumiliki gari yako
mwenyewe, ama kama una ndoto za kusoma zaidi, wewe kazana huku
ukimtumainia Mungu, maana hatakuacha.
Msami kwa hivi sasa, yuko jijini New York nchini Marekani Radio ya
Umoja wa Mataifa, yaani UN Radio idhaa ya Kiswahili akiwa ni muandaaji
wa vipindi na mtangazaji wa radio hiyo , lakini kufika kwake hapo
ni kutokana na kumuamini Mungu na kutokata tama, ikiwemo kujituma. Ni
kama siku moja, kipindi akiwa na shirika la utangazaji wa BBC, kitengo
cha Media Action, aliishiwa pesa, na kupiga mahesabu, akaona ni heri
pikipiki yake aina ya Bajaj akabebea abiria wawili watatu siku iende. Na
hilo lilifanikiwa, kazi ni kazi, hakuna cha umaarufu.
![]() |
Taarifa ya habari inaletwa kwenu na Josep Msami... |
KWA TAARIFA YAKO, mpaka kuja kufikia kuwa mtangazaji mzuri ni kutokana pia na mawazo aliyokuwa nayo tokea utotoni, na hata kugombana na watoto wenzake ili mradi tu asikilize taarifa ya habari. Lakini siku moja, aliipata fresh baada ya kuchapwa sana na mama yake kutokana na kuifungua Redio ili akutane na hao watangazaji anaowasikia kupitia spika. Msami anasema kwamba baada ya hapo, hakurudia tena, ingawa pia mama yake alimnunulia Redio baada kuona kilicho ndani yake.
![]() |
Hapa ni kukamilisha usajili |
Kuufikia U-MC sio shughuli ndogo, lakini aliamini kuwa angeweza
kufanikiwa hasa kutokana na kuwa na ushawishi kipindi anapoongea na
watu, kuanzia utotoni, mpaka kwenye ukonda, basi akaja kuona kumbe kitu
kama hiki kinawezekana. Basi hata uniform za U-MC (viatu) vikatafutwa,
na KWA TAARIFA YAKO hivi sasa Msami ni MC ambaye hutojuta kumuita
kwenye sherehe yako. Na kuthibitisha hilo, siku ya harusi yake, MC
aliyekuwepo alikuwa na kazi ndogo tu, kwani Bwana Harusi alikuwa
mchangmshaji kuliko.
![]() |
Mguu sawa, cadet ndani ya soksi, buti la kazi nje, tayari kwa shughuli ya U-MC |
Pamoja na yote ambayo amepitia, ushauri mkuu anaoutoa kwa makondakta
wenzake, na kila aina ya mtu amaye anahisi kukata tama ya maisha ni
kwamba, ni marufuku kukata tamaa, na huwezi kufikia lengo lako bila
kujaribu.
Na kwa kumalizia ni kwamba, KWA TAARIFA YAKO Joseph Msami ni Refa
mwenye leseni, ni mwanamichezo, captain wa WAPO SC, Mwandishi wa
habari, muendesha bodaboda wa dharura (ambaye muda mwingine inalazimika
kusukumwa
* sio tatizo la mafuta) na pia ni MC, na mtafsiri
mzuri tu wa mahubiri ya lugha ya kiingereza. Haya yote anasema, kama si
kumtumainia Mungu, basi hakuna ambacho kingewezekana.![]() |
Captain Msami akimtambulisha mgeni rasmi mwakilishi wa Kamanda wa kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, Marietha Komba, kikosi cha WAPO SC |
![]() |
Producer wa duru za michezo akipokea maagizo kutoka kwa Mhariri Mkuu, wiki moja kabla ya harusi ni ubize kwa kwena mbele |
No comments:
Post a Comment