
Msichana mmoja, Mariam Chacha, mkazi wa Mtaa wa Nyasho A, mjini hapa amemwagiwa maji ya moto na kuunguzwa mwili, hali iliyofanywa alazwe katika hospitali ya mkoa.
Tukio
hilo la kusikitisha lilitokea Oktoba 22 mwaka huu saa mbili usiku
ambapo inadaiwa aliyefanya kitendo hicho ni Pendo Wambura ambaye
amekamatwa na polisi.
Habari
kutoka ndani ya kituo cha polisi mjini hapa zinadai kuwa mara baada ya
Mariam kumwagiwa maji ya moto na mwenzake na kuungua sehemu za kitovu
mpaka usoni, matiti na mikono na akiwa hajitambui mpaka sasa, wasamaria
wema walimpeleka polisi ili kupata hati ya matibabu (PF 3) na akaenda
kutibiwa katika Hospitali ya Serikali ya Musoma alikolazwa wodi namba
nne.
“Polisi
tulikwenda kumkamata mtuhumiwa na tunamshikilia kwa kuwa majeruhi hali
yake ni mbaya, kalazwa, na tayari amefunguliwa jalada namba
MUS/IR/5009/013,” alisema afisa mmoja wa polisi kwa sharti la
kutoandikwa jina lake gazetini kwa kuwa siyo msemaji.
Shuhuda
mmoja aliliambia gazeti hili kwamba Mariam alikwenda kuwasalimia ndugu
zake pamoja na mama yake ambaye ni mgonjwa wanaokaa nyumba moja na
mtuhumiwa.
“Mariam
alipoona hali ya mama yake alianza kulia ndipo Pendo alipokwenda
kuchukua maji yaliyokuwa yakichemka ili yapikiwe ugali wa mama mwenye
nyumba na akamwagia mwenzake akidai eti anachukizwa na kitendo chake cha
kumlilia mgonjwa wake,” kilisema chanzo.
No comments:
Post a Comment